Thursday, 14 April 2011

Kuondoa Chunusi/Vipele Matakoni.

Watu wengi upata chunusi kwenye makalio. Maeneo ya kawaida kupata chunusi au vipele ni usoni, shingoni, mikono, kifuani, mgongoni na kati kati ya mapaja. Hata hivyo vipele vinaweza kutokea mahali popote. Asilimia themanini ya watu upata chunusi/vipele kwa wakati fulani. Wanaume nao upatwa na chunusi ila ni kwa kipindi kifupi lakini wanawake upata chunusi kwa muda mrefu sana.

Njia bora ya kuondoa chunusi ni kupandana na vitu vinavyosababisha chunusi na kupata matibabu. Sasa tuangalie sababu ya chunusi (ikiwa ni pamoja na chunusi kwenye makalio), na kisha matibabu ya ufanisi zaidi ya kuondoa na kupunguza chunusi. Kwa kufuata ushauri huu, utopata chunusi kwenye makalio au mahali popote.Sababu ya chunusi kwenye makalio.
Hakuna sababu ya uhakika kuhusu sababisho la chunusi kwenye matako ambayo imethibitishwa hadi sasa. Wengi wanaamini kwamba uvaaji wa nguo mara kwa mara ambao hauruhusu ngozi kupumua inasababisha chunusi kwenye makalio. Inawezekana sababu nyingine ya chunusi kwenye makalio ni pamoja na: Baadhi ya Dawa au Sabuni, kutokuosha mashuka na nguo mara kwa mara, stress, chakula, kutokuweka mwili wako safi na homoni.
Chunusi/Vipele zinaweza kuathiri mtu yeyote. Vijana au wazee, mweusi au mweupe, mwanamume au mwanamke, mtu yeyote anaweza kuathirika na Chunusi au Vipele.

Sababu nyingine ni pamoja na:
Umri. Mabadiliko ya Homoni kwa vijana kikawaida yanaweza kusababisha chunusi.
Magonjwa. Magonjwa mengi yanaweza kusababisha mabadiliko ya homoni, ambayo usababisha chunusi.
Mabadiliko ya Homoni. Hasa kwa wanawake yanayohusiana na hedhi au ujauzito.
Diet. Kula kwa afya usaidia mwili wako wote. Baadhi ya vyakula vinaweza kusababisha flare-ups ya chunusi, sana sana vyakula vya mafuta.
Usafi Binafsi (Personal hygiene). Kusafisha sehemu moja mara nyingi ni hatari kwani sabuni nyingine ni kali kwa ngozi na zinaweza kukuchubua au kukuletea vipele, na kushikashika au kukuna vipele usababisha ukuaji kuongezeka zaidi. Hii ni sababu kuu mojawapo ya kupata vipele matakoni
.
Mazingira. Hali ya hewa, uchafu, na jasho usababisha vipele katika ngozi yako.
Stress. Stress inaweza kusababisha matatizo mengi ikiwa ni pamoja na chunusi.
Kutumbua/kubinya Chunusi. Hii itafanya ngozi yako kuwa na uwezekano wa kuendeleza zaidi vipele/chunusi na inaweza kusababisha madoa au makovu.


Kwa kwa kuepuka kufanya vitu vinavyosababisha uongezeko wa chunusi, basi vipele vitaacha kuongezeka kwa asilimia kadhaa kwa kufanya hayo na kwa kutumia matibabu unaweza kupunguza au kuondoa chunusi kwenye matako na pia chunusi katika maeneo mengine ya mwili wako.

Matibabu fanisi zaidi ya chunusi kwenye makalio ni kufuata hatua mbili zifuatazo:
Hatua ya Kwanza.
Hatua ya kwanza ni kuosha kwa taratibu na kusafisha eneo lililoathirika mara kadhaa kwa siku. Ni muhimu kuosha na cleanser iliyo bora zaidi. Imeonyesha kuwa cleanser bora na nzuri yafaa iwe na vitu muhimu vifuatavyo: 
Lappa Arctium: utumika kwa ajili ya matibabu ya ngozi yenye vipele au chunusi sugu.
Bulbine Frutescence: usaidia kuzuia maambukizi ya ngozi, uponyaji wa chunusi na matatizo mengine ya ngozi. Pia kulinda ngozi zaidi ya bakteria.
Lavender Essential Oil: Lavender utumika kutibu vidonda na kuzuia makovu. Ni inajulikana kwa ajili ya kutibu chunusi kwenye makalio.
Azadirachta Indica: utumika kwa ajili ya kupambana na bakteria pamoja na kupambana na uchochezi. 
Melaleuca Alternifolia (Tee Tree Oil):  Utafiti umeonyesha kuwa inauponyaji wa kipee kutokana na kupambana na bakteria, vimelea na Septic. Ni moja ya mafuta ya kipekee ambayo yanaweza kutumika bila kukuretea muwasho au kukausha ngozi yako.
Napendekeza kwa wasomaji wangu wote ili kuwa na mafanikio mazuri katika ngozi yako, jaribu kutumia CleanSkin Wash .Kutumia hii cleanser ni dhahiri itakusaidia kuondoa chunusi katika makalio na mahali popote.

Hatua ya Pili.
Hatua ya pili ni kwa kutumia tiba ya chunusi au vipele mara kadhaa kwa siku. Utafiti umeonyesha kuwa dawa ya chunusu iwe na vitu muhimu vifuatavyo: 

Oleum Melaleuca: Utafiti umethibitisha kwamba upambana na microorganisms ambao usababisha maambukizi ya ngozi kama vile chunusi. 
Lavandula Oleum: ni maalumu kwa ajili ya uponyaji na imekuwa ikitumika kwa karne kuponya na kuzuia makovu na kutibu vidonda. 
Calendula officinalis: ni mitishamba ambayo ina nguvu ya kutuliza, pia ni antiseptic na ni anti-inflammatory  na upambana na uchochezi wa chunusi na uponyaji wa ugonjwa wa ngozi. 
Symphytum: utumiwa kwa uponyaji na kwa ajili ya cell regeneration, ni muhimu kwa ajili ya kutibu makovu na ugonjwa wowote wa ngozi.
Pia ziwe na Chlorocresol B.P au Gentamicin Sulphate na nyinginezo.
Hakuna sababu ya kuwa na chunusi kwenye makalio. Kama unataka kuondoa chunusi, fuata maelezo na unahitaji kupata matibabu.

Matibabu ya Chunusi/Vipele.
Kuna maelfu ya dawa zinapatikana lakini inachukua muda kupata matokeo na ni muhimu kupata matibabu bora kwa mara moja na si kupoteza muda na fedha kwa kujaribu matibabu tofauti.
Matibabu haya ni bora kwa chunusi popote kwenye mwili wako.  Kwa sababu ufanya kazi kwa kasi na pia uondoa madoa, na hakuna madhara hatari upande wa dawa kama BENZOYL PEROXIDE.
Na pia unywaji wa maji ni muhimu sana kwa ngozi yako, jitahidi kunywa angalau glass 8 za maji kila siku.
Dawa Nyingine ni: 
SONADERM-GM, 
GENTRISONE cream, 
OXY 10 Acne Lotion. 
OXY 10 Acne Pimple Medication.
ELYCORT.
ClearSkin-A Gel.
Retin A.


Kama una maswali yoyote kuhusu chunusi kwenye matako, tafadhali uliza au tuma email. Kumbuka hakuna sababu ya kuwa na chunusi kwenye makalio wakati matibabu yapo yanapatikana.

Toa maoni tuambie njia au dawa nyingine zinazosaidia.

5 comments:

 1. Mmmmmh i cant believe people have pimple in their butts, thanks God i have a nice skin. I like the article though.

  ReplyDelete
 2. Mi nataka msaada nina chunusi kwenye makalio mpaka naona aibu mista akinitouch kwenye ass mi nid ur help guyz!!!

  ReplyDelete
 3. big ass n beauty nipples20 September 2013 at 02:43

  Mniambie na dawa ambazo ztawah kuniponyesha haraka

  ReplyDelete
 4. mm rashes zimejaa zinaniwasha nakosa amani kabisa .. msaada please contact

  ReplyDelete