Tuesday 5 April 2011

Unyoaji wa Mavuzi.

Moja ya sababu ya kunyoa mavuzi ni kufanya kuwe na muonekano mzuri. Wanawake unyowa ili kuondoa mavuzi yanayonekana wakati amevaa vazi la kuogelea au bikini. Uvaji wa thong au g-string ni sababu nyingine kwa ajili ya kunyoa. Na pia mavuzi unyolewa kwa nia ya kumuamasisha mpenzi kimahaba zaidi.


 Maelezo.
  1. Amua kama unataka kuondoka zote, kupunguza kiasi au kunyoa kimitindo. 
  2. Chagua mahali pa kunyolea kama ni bafuni basi ni vizuri zaidi. Kama mahali pengine, weka bakuli ya maji moto na taulo.
  3. Vua nguo. Unaweza kubaki uchi kabisa au unaweza tu kuondoa sketi/suruali yako na chupi.
  4. Kama huko bafuni simama na weka mguu mmoja upande na hivyo unaweza kupata maoneka wa wazi wa nyeti zako. Kama huko mahali pengine, kaa na tanua miguu yako.
  5. Chukua kioo na angalia pale unataka kunyoa. Kioo kita kusidia kuona vizuri wakati wa kunyoa.
  6. Kama unatumia mkasi, kata nywele karibu na ngozi kama iwezekanavyo.
  7. Mashine za umeme ni bora kwa kukata nywele zako kwa lakini usieweke speed kubwa.
  8. Lowanisha mavuzi yako na maji ya vuguvugu (Sio ya moto)
  9. Paka sabuni au shaving cream nyeti zako. Hakikisha eneo hilo ni safi kabla ya kuanza kunyoa. Kuwa makini na sabuni unayotumia si kupaka sabuni yoyote katika nyeti zako.
  10. Safisha uke wako katika maji ya moto tena.
  11. Rudia hatua ya 4. (Simama mguu upande au kaa na kupanua miguu).
  12. Paka sabuni au Shaving Cream (sehemu ya juu ya nyeti zako ambapo nywele hukua zaidi), na kaa kwa dakika chache.
  13. Anza kunyoa na nyoa kinyume na ukuaji wa nywele. Nyoa kwenda juu.
  14. Paka tena sabuni au shaving cream na nyoa sideways ili kukata nywele zote.
  15. Kwa makini nyoa upande mmoja wa labia/pumbu yako kwa utaratibu kuepuka kujikata.
  16. Rudia hatua ya juu kwa upande wa pili wa pumbu/labia yako
  17. Ukimaliza kunyoa jifute shaving cream au sabuni na nguo mbichi au yenye maji kidogo.
  18. Safisha nyeti zako na maji ya moto kiasi. Safisha sehemu uliyonyolea nywele kisha waweza oga.
  19. Paka moisturizer after shave ili kupunguza msisimko wa kuwasha na vipele.
  20. Nyoa tena kama inahitajika au zitakapoota.


Maelezo Zaidi.
Kunyoa
Kwa ajili ya afya na usalama unahitaji kutumia wembe safi kwa kunyoa. Fikiria kazi hii ni kama kukata nyasi pale zinapoota na kuwa nyingi. Waweza tumia mkasi mkali, wembe au mashine za umeme kufanya kazi hiyo ya kunyoa.

Baadhi ya sabuni zenye marashi sio nzuri kwa kunyolea. Tumia moisturizer yenye vitamini E. Jaribu kukanda eneo ulilonyoa na kipande cha barafu (Ice Cube) juu ya ngozi yako na kisha futa (pat dry) eneo eneo liwe kavu na kitambaa safi. Hii na njia ya kutuliza asidi SALICYLIC na kuzuia nywele zitazoota kutoa vipele au kuotea ndani (Ingrown Hair).

Waxing.(Nta) 
Hii ni njia ya Imara zaidi ya kuondoa nywele na tofauti na ile ya kunyoa nywele kutokana na kuchukua muda mrefu kukua. Ushauri bora ni kuwa fanya Wax kwa mtaalamu. Waxing Kits kwa ajili ya matumizi ya nyumbani inaweza kununuliwa kutoka kwa duka la dawa. Wax inauma kidogo kama si mzoefu lakin haitakuletea muwasho kama vile ukinyoa.

2 comments:

  1. Aise umefanya jambo la msingi kweli. Thanks!!

    ReplyDelete
  2. U have done agreat job for advising us how to play precious and pleased sex with our partners, we conglatulate u but we encourage u to give us more styles within ua blog Vile nataka. Congratulation

    ReplyDelete